×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC KAGANDA AIBUA FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amewataka wawekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika Wilaya ya Babati, hususan kwenye sekta ya utalii kwani Wilaya hiyo imebarikiwa vivutio vya kipekee vyenye uwezo mkubwa wa kuchochea uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ametaja miongoni mwa vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Mlima Kwaraa unaofaa kwa shughuli mbalimbali za kitalii kutokana na uwepo wa mandhari nzuri inayovutia watalii, ambapo wawekezaji wanaweza kujenga nyumba za wageni na kuweka huduma bora za kitalii.

Sambamba na hilo, Pia Kaganda ametaja uwepo wa ziwa Babati kama kivutio kizuri chenye fursa kubwa ya uwekezaji, kwa ujenzi wa hoteli na shughuli za mapumziko, hususan utalii wa picha.

Vilevile, ameeleza kuwa maeneo yanayozunguka hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ziwa Manyara tayari yameanza kunufaika na miradi ya kiuchumi, akitaja mfano wa uwepo wa mradi wa ufugaji wa kuku wa biashara uliozinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata kipato kupitia mifugo hiyo.

#NTTupdates.