×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC TEMEKE AFUNGA CHUO,AAGIZA MKUU WA CHUO KUKAMATWA

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda Novemba 21, 2024 amekifungia Chuo cha Kewovac kinachojihusisha na utoaji wa Elimu ya Uuguzi na Ukunga kilichopo Mbagala Charambe kwa kutokidhi vigezo vya utoaji wa elimu hiyo na ubovu wa mazingira ya Chuo hicho.

DC Mapunda ameagiza kukamatwa mara moja kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho na wasaidizi wake ili kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwemo kukiuka agizo la serikali kukifungia Chuo hicho hadi pale kitakapoweka mazingira rafiki kwa ajili ya wanafunzi kusomea

“Ofisi inayosimamia uendeshaji wa vyuo hivi, ukichunguze chuo hiki vizuri, ninafunga rasmi kituo hichi leo hii kuanzia sasa hakitatoa huduma” alisema Dc Mapunda

Makosa mengine yanayomkabili Mkurugenzi huyo ni Pamoja na kutofuata mtaala wa Serikali unaoagiza elimu ya uuguzi na ukunga kufundishwa kwa miaka miwili na si mwaka mmoja kama kinavyofanya chuo hicho.

#NTTUpdates