×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DE BRUYNE ATANGAZA KUONDOKA MAN CITY

Na Mwandishi wetu.

Nahodha na Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne (33), raia wa Ubelgiji ametangaza rasmi kupitia mitandao ya kijamii kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwatumikia kwa miaka 10.

De Bruyne ambaye amejiunga na Manchester City mwaka 2015 akitokea VfL Wolfsburg ya Ujerumani amekuwa mchezaji tegemezi kwenye eneo la kiungo la klabu hiyo kutokana na uwezo wake wa kunyumbulika na kutoa pasi sahihi eneo la ushambuliaji.

Akiwa Manchester City De Bruyne ameshinda mataji 6 ya EPL, taji 1 la ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) na kuondoa uteja wa klabu hiyo kwa kushindwa mara kadhaa kubeba kombe hilo, pia ameshinda kombe moja la klabu bingwa ya Dunia.

Licha ya kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha lakini msimu huu De Bruyne amecheza michezo 31 akifunga magoli 5 na kutoa assist 7 kwenye michuano yote ambayo Manchester City imeshirikia hadi sasa huku vilabu kutoka Saudi Arabia vikionekana kumuhitaji nyota huyo.

#NTTupdates