Na Mwandishi wetu.
Mwendesha pikipiki maarufu kama(Bodaboda) Bernado Masanja mkazi wa Mtaa wa Tambuka reli mkoani Shinyanga Bernado Masanja (24) amechomwa na kisu na kisha kupoteza maisha na mwendesha pikipiki mwenzake, aliyefahamika kwa jina moja la Kulwa ambapo tukio hilo limesababishwa na ugomvi wa wakugomvania abiria katika kituo chake cha kazi.
Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amesema kuwa, mauaji hayo yalitokea June 22 majira ya Saa sita usiku ambapo Marehemu alichomwa na kisu kisha wauaji wakatokomea kusikojulikana.
Jeshi la Polisi limesema kuwa, linaendelea na msako mkali kumtafuta mtuhumiwa huyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Jeshi la Polisi limetoa wito Kwa wananchi wote kuacha kujichukulia sheria mkononi, maana kufanya hivyo ni kinyume cha sheria huku akibainisha ni vyema wazazi na Walezi kuwekeza zaidi katika malezi imara na bora Kwa watoto wakiwa bado wadogo ili kuondoa vitendo vya kikatili.
#NTTUpdates