×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 KUZINDULIWA KESHO.

Na Mwandishi wetu.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho Disemba 9, 2023 anatarajiwa kuzindua maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inalenga kuweka muktadha wa maendeleo ya Kitaifa katika mwelekeo wa makubaliano na mipango ya Kikanda na Kimataifa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuelezea kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na Mkutano wa Kwanza wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

“Shughuli za maandalizi ya maadhimisho haya zinaendelea vizuri na ya mwaka huu hatutafanya tu maadhimisho kama ilivyozoeleka lakini itakuwa tofauti ambapo tutaungana na wenzetu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji kufungamanisha na Dira ya Maendeleo ya Taifa tutaanza 2025 hadi 20250. Miaka 62 ya Uhuru wetu imebebwa na kauli mbiu ya Umoja na Mshikamano ni chachu ya Maendeleo ya Taifa letu,” Amesema Mhe. Ummy.Mhe. Ummy

Ameongeza kwamba kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya smwaka 2025 yapo mafanikio mengi ambayo yamepatikana yakiwemo sekta ya elimu kuimariska, Afya pamoja na uwezeshaji wanawake katika maeneo mbalimbali.

“Liko eneo la kuwawezesha wanawake leo tunaye Rais mwanamke jasiri na mahiri Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo tunaendelea kumpongeza kwa miongozo na maelekezo yake ambayo yameleta mfungamano huu pamoja na utayari na utashi wake wa kisiasa,”Ameeleza.

Kadhalika alisema uzinduzi huo utafanyika kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

#NttUpdates