×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DKT. MPANGO AAGIZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KULINDWA

Na Mwandishi wetu.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, ametoa wito kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii barani Afrika kuhakikisha kwamba michango ya wanachama inahifadhiwa kwa uangalifu kama kinga dhidi ya mabadiliko ya kiuchumi, na inabaki kuwa ya kutosha kufikia malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake.

Dkt. Mpango amezungumza hayo hii leo Julai 10, 2025 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Kimataifa wa watunga sera wa sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Aidha, amebainisha kuwa uwekezaji wa mifuko hiyo katika miradi ya maendeleo ya miundombinu unaweza kuhatarisha majukumu yake ya msingi ya kutoa ulinzi wa kijamii kwa makundi yaliyo hatarini kama vile wastaafu, wagonjwa, na watu wenye ulemavu hivyo Mamlaka husika zinapaswa kuwa na mipango mikakati ya kukabiliana na hali ya aina yoyote inayoweza kujitokeza hasa katika eneo la kiuchumi.

Sambamba na hilo Dkt. Mpango amesisitiza kuwa miradi inayowekewa mitaji inapaswa kuwa na tija ya kiuchumi na kifedha ili kuepusha ucheleweshaji wa mafao au kutoweza kulipa kabisa kwa wanachama wa mfuko huo.

#NTTupdates.