ร—
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DURAN MCHEZAJI GHALI ZAIDI UTURUKI

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Al Nassr FC imetangaza kumpeleka kwa mkopo wa mwaka mmoja mshambuliaji wao Jhon Jader Duran Palacios (21) raia wa Colombia kwenye klabu ya Fenerbarhce ya Uturuki.

Duran ambae alijiunga na Al Nassr dirisha dogo msimu uliopita akitokea Aston Villa ya Ligi kuu Uingereza (EPL), na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi nyuma ya Cristiano Ronaldo huku akiwa mchezaji ghali zaidi kwenye ligi hiyo.

Mshambuliaji huyo amekubali kujiunga kwa mkopo na Fenerbarche ya ligi kuu Uturuki na kutajwa kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye ligi hiyo akiwa na thamani ya paundi Milioni 35 akifuatiwa na mjerumani Lorey Sane mwenye thamani ya paundi Milioni 32.

Jhon Duran aliichezea Al Nassr FC jumla ya Michezo 18 akifunga magoli 12 licha ya timu hiyo kushindwa kubeba ubingwa.

#NTTupdates