×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

EDERSON AWEKA REKODI YA KIPEKEE EPL

Na Mwandishi wetu.

Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Manchester City, Ederson Santana de Moraes (31), ameendelea kuandika historia ya kipekee kwenye ligi kuu Uingereza (EPL) baada ya kuweka rekodi ya kuwa goli kipa pekee mwenye assist nyingi kwenye ligi hiyo akimwacha mbali Paul Robinson mwenye assist 5.

Ederson ameweka Assist yake ya 7 leo kwa McAtee kwenye mchezo wa ligi kuu EPL kati ya Manchester City dhidi ya Crystal Palace ambapo mchezo huo uliisha kwa Man City kumpata ushindi wa magoli 5-2.

Msimu huu hadi sasa Ederson amecheza michezo 32 akiruhusu magoli 42 huku akiwa na Clean sheet 9 pekee kwenye mashindano yote ambayo Manchester City imeshiriki.

#NTTupdates