Na Mwandishi wetu.
Baada ya tukio la kuhuzunisha kwa kiungo wa Fiorentina, Edoardo Bove (22) raia wa Italia kudondoka uwanjani hapo jana na kupoteza fahamu baada ya kupata shambulio la moyo na kupeleka mchezo wa ligi kuu Italia Serie A, kati ya Fiorentina na Inter Milan kughairishwa na kiungo huyo, kupakiwa kwenye gari ya wagonjwa na kukimbizwa katika Hospitali na Careggi huko Florence nchini Italia.
Taarifa njema ni kuwa kiungo huyo ambaye alikuwa kwenye chumba Cha wagonjwa mahututi amerejesha fahamu na mapigo yake ya moyo yameimarika.
Klabu ya Fiorentina imewashukuru mashabiki na vilabu mbalimbali ambavyo vimeonyesha kuguswa na tukio hilo la kuhuzuni kwa kiungo huyo na ikiendelea kuwaomba waendelee kumuombea apone haraka ingawa bado yupo chini ya uangalizi wa Madaktari kwenye Hospitali hiyo.
#NTTupdates