×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

EDWIN BALUA APELEKWA CYPRUS KWA MKOPO.

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Simba SC imetoa taarifa rasmi ya kumtoa kwa mkopo kiungo mshambuliaji wao Edwin Charles Balua (24) kwenda nchini Cyprus kujiunga na klabu ya Enosis Neon Paralimniou FC ya ligi kuu nchini humo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Balua ambae alijiunga na Simba SC msimu uliopita akitokea kwa Wajelajela Tanzania prisons ya jijini Mbeya, atakumbukwa kwa goli kali kwenye mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya dakika za Jioni.

“Tunaendelea kuwa na utaratibu wa Kuruhusu wachezaji wetu kujiunga na timu zinazowahitaji hasa za kimataifa, kila wanapohitajila ikiwa ni kwa faida yao na kwa manufaa ya Taifa kiujumla”

Imeeleza taarifa ya Simba SC kupitia Simba SC App.

Credit📷Simba SC

NTTupdates