Na Mwandishi wetu.
Mshambuliaji wa klabu ya Intenacional na timu ya Taifa ya Ecuador, Enner Remberto Valencia Lastra (34), ameingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye michuano ya Copa America 2024 kupewa kadi nyekundu dakika ya 22.
Valencia alipewa kadi hiyo baada ya kumchezea madhambi mlinzi wa timu ya Taifa ya Venezuela Jose Martinez, baada ya kumkita na mguu kwenye kifua wakati akiwania mpira na mlinzi huyo.
Kadi nyekundu hiyo ilipelekea Ecuador kucheza pungufu na kupokea kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Venezuela, pia Enner Valencia atakosa michezo yote miwili iliyobakia hatua ya makundi kutokana na kadi hiyo.
#NTTupdates