Na Mwandishi wetu.
Shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza rasmi kuwa fainali ya kombe la FA la CRDB itapigwa Visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa New Amaan Complex.
Fainali hiyo itapigwa Juni 28, 2025 saa 2:15 na itakuwa ya pili mfululizo kupigwa Visiwani Zanzibar ambapo inawakutanisha Young Africans SC dhidi ya Singida Black Stars.
#NTTupdates