×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

FAMILIA YA HAYATI EDWARD LOWASSA YAFANYA IBADA MAALUM YA SHUKRANI

Na Mwandishi wetu Arusha.

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mhe.John V.K Mongella,amesema Hayati Edward Lowassa atakumbukwa na wakazi wa Mkoa wa Arusha kutokana na uzalendo na uchapakazi wake, ambao umechangia maendeleo na mafanikia ya Mkoa wa Arusha.

Mongella anasema hayo, wakati akitoa salamu za Mkoa wa Arusha, kwenye ibada Maalum ya Shukrani ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowasa, iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Monduli Machi, 24, 2024.

Anasema kuwa, Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Arusha, Hayati Edward Ngoyai Lowassa ataendelea kukumbukwa kwa mambo makubwa aliyoyafanya mkoani Arusha, ikiwa ni pamoja na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya Mkoa na wananchi wa Mkoa wa Arusha.

Aidha, ameishukuru familia kwa kuwakaribisha kwenye ibada hiyo muhimu, licha ya kutoa pole kwa familia amewataka wanafamilia kuendelea kumtegemea Mungu.

Awali, familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa imeandaa ibaada ya shukrani, kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Monduli ibaada iliyoongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazin Kati, Mchungaji Lareton Loishiye.

#NTTUpadates