Na Mwandishi wetu.
Mtendaji Mkuu (CEO) wa Shirika la Abbot Fund, Robert Ford, ameridhidhishwa na utekelezaji wa mradi wa maabara ya ujuzi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Akiongea leo, Ndg. Ford, ameahidi kuwa Abbot Fund itaendelea na ushirikiano na BMH.”Hii ni Hospitali namba moja hapa Dodoma
Inabidi mjivunie kuwa na hii Hospitali,” amesema C.E.O wa Abbot Fund wakati wa ziara yake BMH.Shirika la Abbot Fund waligharamia ujenzi wa maabara ya ujuzi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa thamani ya 400m/-. Maabara hii imezinduliwa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, mwezi Septemba.Kwa upande, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Kessy Shija, amesema ujenzi wa Maabara ya Ujuzi umeanza mwishoni mwa mwaka jana.
“Mradi wa Maabara ya Ujuzi umekamilika mwanzoni mwa mwaka huu na tumekabidhiwa mwezi Machi,” amesema Dkt. Shija kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof Abel Makubi.
Dkt. Shija amesema Maabara hii ya Ujuzi itakuwa na manufaa sana kwa watumishi wa Afya kutoka idara za huduma ya dharura.”Washiriki ishirini wataweza wataweza kushiriki mafunzo kwa awamu moja.
Kituo kitakuwa na manufaa sana kwa watumishi wa Afya kutoka idara ya dharura,” amesema Dkt Shija.
#NTTupdates