Na Mwandishi wetu.
Mmoja wa Nyota mahiri zaidi wa filamu huko Hollywood, Walter Bruce Wills ameendelea kuwa katika hali mbaya ya Kiafya na kupelekwa kwenye nyumba ya utunzaji, huku vita vyake dhidi ya shida ya akili ya frontotemporal inazidi kuwa mbaya.
Bruce mwenye umri wa miaka 70, hawezi tena kuongea, kusoma, kuandika, kutembe na amepoteza kabisa kumbukumbuka kuwa hapo awali alikuwa mwigizaji wa hadithi na maarufu Duniani.
Mkewe Emma Wills ameweka wazi kuwa alifanya uamuzi huo wa kumpeleka kwenye nyumba za utunzaji kwa kuwa ndicho ambacho Mabinti zao walikuwa wakihitaji ingawa wamehuzunishwa sana.
Bruce Wills aliwahi kutamba na filamu nyingi za mapigano (Action Movies) kama Die Hard (1988), Red (2010), Death Wish (2018), American Siege (2021), Paradise City (2022), Vendetta (2022), Wrong place (2022),Wire Room (2022), A Day to Die (2022) na Detective Knight (2023)
.#📷 Brucewillis.
#NTTupdates.