×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

IBADA MAALUM YA KUMUOMBEA HAYATI DKT JOHN MAGUFULI CHATO

Na Mwandishi wetu.

Viongozi wa Umma wametakiwa kuongoza nchi kwa haki na kuimarisha upendo kwa jamii ili kumuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania,Hayati Dkt. John Pombe Magufuli(JPM) aliyefariki Machi 17,2021 wakati wakipatiwa matibabu ya matatizo ya umeme wa moyo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam.

Kadhalika wametakiwa kuendelea kujifunza mema kutoka kwake kutokana na moyo wa uzalendo wa kuipenda nchi yake na kuhakikisha analinda kwa moyo wa dhati raslimali za taifa.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi,ameyasema hayo wakati akiongoza Ibada maalumu ya kumbukizi ya miaka minne ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli, huku akiwataka wote waliochukizwa na kwa namna yoyote na utawala wake wamsamehe kwa kuwa ndiyo siri ya kuvuna baraka za Mwenyezi Mungu.

“Dkt. Magufuli alikuwa ni mwanadamu na kwaniaba yake mimi ninaomba kwa mabaya yoyote aliyotenda tumsamehe maana hayupo tena Duniani, na wasioweza kumsamehe mimi ninasema hao siyo wakristo” amesema Askofu Niwemugizi.

Katika Ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Mariamzei Mlimani Rubambangwe Chato, na kuongozwa na Askofu Niwemugizi, pia imetumika kutoa pole nyingi kwa mjane wa marehemu, Mama Janeth Magufuli pamoja na familia yote kwa ujumla kwa kuondokewa na mume na Baba wa familia na kwamba wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo kwa kuwa ni mpango wake kwa wanadamu.

Pamoja na mambo mengine,amesisitiza kila mmoja kuandika kitabu chake vizuri kingali bado hai,huku akisisitiza kuwa kila mwaka Kanisa litaendelea kumwombea Hayati Magufuli kutokana na mchango wake mkubwa kwa Kanisa na taifa kwa ujumla.

Kadhalika amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutuma uwakilishi wake katika ushiriki wa maadhimisho ya ibada hiyo na kwamba watanzania wanapaswa kuendelea kuishi kwa upendo na mshikamano.

Katika Ibada hiyo,viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wamehudhuria akiwemo mwakilishi wa Rais Samia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu,William Lukuvi, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Innocent Bashungwa.

#NTTUpdates