Na Mwandishi wetu
Kikosi maalumu cha kuzuia Magendo Visiwani Zanzibar (KMKM),kimempandisha cheo askari wa kikosi hicho ambaye pia ni mlinzi wa kati wa klabu ya Young Africans SC na timu ya Taifa ya Tanzania Ibrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka cheo cha Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora uwanjani akiwatumikia wananchi.
Ibra Bacca ambaye amekuwa mlinzi muhimu kwenye kikosi cha wananchi Young Africans SC huku akisifika kwa umahiri wake wa kuwadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
#NTTupdates