×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

IDADI YA VIFO KUTOKANA NA SHAMBULIO LA ISRAELI IMEONGEZEKA HADI 9

Na Mwandishi wetu.

Idadi ya vifo kutokana na shambulio la angani la Israeli , Beiruti Kati mapema leo Alhamisi imeongezeka hadi tisa, wizara ya afya ya Lebanon imesema.

Shambulio hilo lilipiga eneo la Bashoura, karibu na katikati ya jiji, CNN ilithibitisha wakati ikipita kuangalia eneo hilo.

Taarifa kutoka kwa wizara ya afya ya Lebanon leo Alhamisi imesema idadi ya vifo imefikia tisa “mashujaa.

“Aidha, watu 14 wamejeruhiwa. Vipimo vya DNA vinafanyika ili kubaini utambulisho wa baadhi ya mabaki.

CNN iliripoti awali kuwa angalau watu sita walikuwa wamekufa katika shambulio hilo.Hii ni mara ya kwanza kwa Israeli kushambulia eneo hilo tangu mwaka 2006.

Shambulio la Israeli limeuwa zaidi ya watu 1,000 nchini Lebanon na kuwahamisha takriban watu milioni 1 tangu vita vyake na Hezbollah vilipoongezeka.

#NTTupdates