Na Mwandishi wetu.
Kwa mujibu wa IGP Wambura Matukio ya uporaji, utekaji na ujambazi yamethibitiwa.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillius Wambura, amesema Mikoa ya Kagera, Kigoma na Arusha ilikumbwa na Matukio ya utekaji, ujambazi na uporaji.
Akiwa Jijini Dar es salaam wakati wa kufunga kozi ya maofisa na wakaguzi wasaidizi Wa Polisi Waliomaliza Mafunzo Yao Katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Kurasini, IGP Wambura amesema tangu kiruhusiwa Kwa magari ya kusafirisha abiria usiku tangu Oktoba 1, Mwaka 2023 hakuna tukio linalohusisha unyang’anyi limeripotiwa.
#NTTupdates