
Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) imemfungia mizunguko mitatu muamuzi Ally Mnyupe kutoka Morogoro baada ya kushindwa kutafsiri Sheria za soka kwenye mchezo namba 104, Kati ya Azam FC dhidi ya Young Africans SC uliochezwa siku ya Jumapili tarehe 15/3/2026 katika dimba la Benjamini Mkapa Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana huku Young Africans SC wakilalamika kwa muamuzi huyo kushindwa kutafsiri Sheria baada ya mshambuliaji Prince Dube kifanyiwa madhambi katika eneo la penati na mlinzi wa kati wa Azam FC Fuentes Mendoza raia wa Colombia
@YoungAfricansSC