Na Mwandishi wetu.
Zimesalia saa chache kushuhudia mchezo mkali wa mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya Al Masry ya Misri kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 10:00 Jioni.
Simba SC wanalazimika kupata ushindi wa kuanzia magoli 3 huku wakitakiwa kuwazuia Al Masry SC wasipate goli lolote kwenye mchezo huo baada ya mchezo wa awali Simba SC kupoteza kwa magoli 2-0 kwenye dimba la Suez canal nchini Misri.
Simba SC ndio klabu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa baada ya timu zote kuondolewa huku wakitaka kuondoa uteja wao wa kushindwa kufuzu nusu fainali kwenye michuano ya kimataifa kwa zaidi ya misimu 6 wakiishia robo fainali kwenye ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na kombe la shirikisho Afrika (CAFCC).
#NTTupdates