Na Mwandishi wetu.
Kipa namba moja wa kikosi cha Fountain Gate FC, John Noble (31), raia wa Nigeria amejikuta kikaangoni baada ya kufanya uzembe kwenye mchezo wa ligi kuu NBC dhidi ya Young Africans SC baada ya kuruhusu magoli 2 kipindi cha kwanza na kupeleka kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na kipa namba mbili Ibrahim Parapanda.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa Fountain Gate FC kupoteza kwa kichapo cha magoli 4-0 kulimfanya Kocha wa kikosi hicho Roberto Matano kutoa lawama zake kwa goli kipa John Noble akimlaumu kwa kuwatoa wenzie mchezoni kutokana na uzembe wake kwenye mchezo huo na kupeleka kuruhusu magoli mawili yaliyofungwa na Clement Mzize na Aziz Ki.
“Magoli ya leo ni ya kupeana, Golikipa ametutoa kwenye mchezo, huwezi ukafanya makosa kama yale halafu utegemee timu kurudi mchezoni”.
“Kwa makosa yale hata Yanga wenyewe wasingerudi mchezoni, Golikipa ametuangusha”Robert Matano Kocha wa Fountain Gate FC akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika.
#NTTupdates