Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Juventus ya Italia imemfuta kazi Kocha wake Thiago Motta Santos Olivares (42) raia wa Italy baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha kwenye kikosi hicho.
Motta ambaye alijiunga na Juventus mwanzoni mwa msimu huu akitokea Bologna hajawa na nyakati nzuri kwenye kikosi hicho baada ya kuiongoza klabu hiyo kwenye jumla ya michezo 42, akishinda michezo 18, akipata suluhu michezo 16 na kupoteza michezo 8 kwenye michuano yote ambayo Juventus imeshiriki msimu huu.
Juventus ipo nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu Serie A baada ya kukusanya alama 52.
#NTTupdates