×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KABOYOKA: KAMATI TUMESIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI WA COASCO.<br>

Na mwandishi wetu Dodoma


MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Naghenjwa Kaboyoka amesema kamati imeuagiza Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kuwasilisha orodha ya wadaiwa sugu wa mikopo ya mfuko.

Kaboyoka ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 23 ambapo amesema hatua hiyo imetokana na Mfuko kuwa na madeni chechefu ambayo asilimia 83 haiwezi kukusanywa.

Amesema Mfuko na COASCO umetakiwa kuwasilisha orodha ya wadaiwa hao na kiwango wanachodaiwa kabla ya saa saba mchana kwa katibu wa kamati huku akisema wamesikitishwa na utendaji kazi usioridhishwa wa mfuko kutokana na kuwa na madeni ambayo yanatishia uhai wa mfuko.

“Baada ya hapo tutajua tunachukua hatua gani tukishaona ni nani na kwa nini wameshindwa kurejesha.”amesema Kaboyoka

Ametolea mfano kuwa kati ya shilingi bilioni zilizotolewa kama mikopo ya pembejeo, sh bilioni 20 ni madeni chechefu yasiyoweza kukusanywa ambayo ni sawa na asilimia 83.

“Unaweza kuangalia, Mfuko wa Pembejeo ambao hautoi pembejeo na unatoa mikopo bado asilimia 83 wameshindwa kukuswanya na hizi ni fedha za umma, fedha za walipakodi sasa kuna haja ya huu Mfuko kuwepo?”

“Ukiangalia kazi za Benki ya Kilimo na huu Mfuko wa Pembejeo wanafanya kazi iliyofanana, kuna sababu gani ya kuwa na Benki ya Mendeleo ya Kilimo na Mfuko wa Pembejeo ambao kazi yao pia ni kutoa mikopo. Kwa kweli utendaji wa mfuko si wakuridhisha wa mfuko.”

Kwa upande wa COASCO, Kaboyoka alisema Kamati inawasiwasi na ushughulikiwaji wa taarifa ya ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika.

“Wasiwasi wa kamati imeona COASCO wakifanya ukaguzi ripoti nani anachukua hatua endapo yatabainika mapungufu, na hii ndio inafanya Utendaji wake usionekani umuhimu wake. Kama kamati hatuoni tija ya mfumo huu.”

Kwa upande wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB), Kaboyoka alisema wanakamati wamekuwa na wasiwasi mkubwa na utendaji kazi wa benki na kushindwa kuwafikia wakulima wadogo.

“Wasiwasi wa wanakamati ni kwamba wakulima wadogo ambao ndio lengo la hii benki hawafikiwi na badala yake wanapewa wakulima wakubwa ambao wangeweza kutumia benki za kawaida za biashara, kwa hiyo pana tatizo kubwa.”

Kaboyoka amesema pia benki hiyo imekuwa ikipitisha fedha kwenye Benki nyingine za biashara ili ziwakopeshe wakulima.

“Sasa tunajiuliza hiyo gharama nani anaibeba. Kamati ina hoji kwa nini hii beki itumie fedha za umma kupeleka kwenye Benki nyingine ili wakulima wetu waende wakachukue huko na riba zile ziende kwa mkulimwa, kwa hiyo tunaona hili si sahihi na haijakaa vizuri.”

Mwisho.