Na Mwandishi wetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha Novemba 18, 2024 imetangaza kutenga Shillingi Billion Moja na Million Mia moja kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 kwaajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Takwimu hizo zimetolewa na Bi. Flora Samwel ambaye ni Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Karatu, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu na Mkurungezi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bw. Juma Hokororo, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la utoaji mikopo ya 10% za Halmashauri.
Kwa upande wake, Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Bw. Juma Hokororo amesema kwa hatua hii ya awali wametoa kiasi cha shillingi million mbili na laki tano kwa vikundi tisa viliyoomba na kukidhi vigezo vimeweza kupatiwa kiasi cha fedha husika.
Aidha, BW. Juma Hokororo pamoja na baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha zoezi hilo lililokuwa limesitishwa hapo awali.
#NTTupdates