×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KARIAKOO DERBY APEWA ARAJIGA

Na Mwandishi wetu.

Bodi ya ligu kuu TPLB imemtangaza mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara ndiye atakayesimamia sheria 17 mpira wa miguu kwenye mchezo mkubwa wa Kariakoo Derby utakaopigwa siku ya jumamosi Machi 8, 2025 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Arajiga ambaye ana uzoefu mkubwa wa kuchezesha mechi kubwa kwenye ligi kuu na michuano mbalimbali ya kimataifa barani Afrika atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam kwenye mchezo huo.

#NTTupdates