×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KARIAKOO DERBY NANI KUTINGA FAINALI NGAO YA JAMII

Na Mwandishi wetu.

Saa chache zimesalia kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya jamii ambao unawakutanisha watani wa jadi Simba Queens dhidi ya Yanga Princess kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam majira ya saa 10:00 Alasiri.

Simba Queens ndio bingwa mtetezi wa Ngao hiyo na wamejipanga kutetea tena taji hilo na kuanza msimu vyema.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya JKT Queens dhidi ya Ceasiaa Queens.

#NTTupdates