Na Mwandishi wetu.
Baada ya taarifa kutoka klabu ya Young Africans SC kuwa hawatacheza mchezo wa Kariakoo derby dhidi watani wao Simba SC mpaka pale matakwa yao yatakaposikilizwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya ligi, Almas Jumapili Kasongo ameweka bayana kuwa wamesikiliza matakwa ya Young Africans SC lakini hayazuii mchezo huo kupigwa juni 15, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Wenzetu Yanga SC leo wamekuja na matakwa ya mambo manne na mambo hayo ni kuvunja kwa kamati ya uendeshaji wa bodi ya ligi (masaa 72), Kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi, kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF na bodi ya ligi iwe huru”
“Mechi ya Juni 15 ipo palepale hayo matakwa yao manne sio rahisi kama inavyotajwa, matakwa yao sio mchakato wa siku moja mfano hili la Bodi ya Ligi kuwa huru na ijitegemee haiwezi kuwa hivyo kwa siku moja”.
#NTTupdates