Na Mwandishi wetu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Joseph Kayombo leo Oktoba 13 , 2025 ameipokea timu ya Madaktari Bingwa wa Mama Samia watakaokita kambi Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za Kibingwa.
Mabingwa hao kutoka Hospitali mbalimbali za Mikoa ya Kanda ya Ziwa watakaokuwepo katika Hospitali zote za Wilaya Mkoani Simiyu kwa muda wa siku saba watatoa huduma mbalimbali za Kibingwa na ubingwa bobezi katika magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya Kinamama, Usingizi, Macho,Kifua pamoja na huduma nyinginezo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Madaktari hao katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katibu Tawala Bi Prisca Kayombo, amewataka mabingwa hao kuhakikisha wanasaidia kutoa elimu na utaalamu wao kwa madaktari wa Mkoa wa Simiyu ili waweze kuwa na uelewa mkubwa wa utoaji wa huduma za kibingwa katika maeneo mbalimbali Mkoani humo.
Aidha amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa anaouonyesha kwa Wananchi kwa kuwasogezea karibu huduma za kibingwa ambazo wakati mwingine Wananchi hao huingia gharama kubwa kusafiri kwenda mbali kufuata huduma hizo za kibingwa.
#NTTupdates.