Na Mwandishi wetu.
Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu, inatarajiwa kuendelea hii leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Hadi sasa tayari ulinzi umeimarishwa na Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam huku waakishuhudiwa Wanachama na Viongozi mbalimbali wa Chama hicho.
Baadhi ya Viongozi hao ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob lakini pia jopo la Mawakili linalomtetea Tundu Lissu, likiongozwa na Mawakili waandamizi Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala, na Peter Kibatala.
Lissu anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube na uhaini.
Awali, kesi hizo zilikuwa zinasikilizwa kwa njia ya mtandao, lakini Mei 6, 2025, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini, alitoa uamuzi wa kumtaka Lissu kufika mahakamani kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo badala ya kuendelea kwa njia ya mtandao huku kesi ya tuhuma za uhaini ikiendelea kwenye mtandao.
#NTTUpdates