×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KILA LA KHERI TAIFA STARS

Na Mwandishi wetu.

Zimesalia saa chache kushuhudia mchezo wa kihistoria wa hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CHAN 2024, kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco “Simba wa Atlas” majira ya saa 2:00 usik, katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Kikosi Cha Taifa Stars chini ya Kocha Hemedi Suleiman kimejiandaa kupambana kwa jasho na damu kwenye mchezo huo na kupata ushindi ili waweze kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali na kuendelea kuandika historia.

Taifa Stars wameweka rekodi ya kufanya vizuri kwenye michuano ya CHAN 2024 kwa mara ya kwanza toka yaanzishwe mwaka 2009, baada ya msimu huu kufika hatua ya Robo fainali wakiwa Vinara wa Kundi B huku wakiwa miongoni mwa mataifa wenyeji wa michuano hiyo.

#NTTupdates