×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KILICHOWAPONZA BRAZIL NI KAMDOMO

Na Mwandishi wetu.

Timu ya Taifa ya Brazil imepokea kichapo kizito cha magoli 4-1 kutoka kwa bingwa mtetezi wa kombe la dunia Argentina, kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2026.

Kabla ya mchezo huo nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Raphinha alitamba kuwa lazima wapate ushindi kwenye mchezo huo na hawana cha kuhofia dhidi ya Argentina.

Raphinha: “Tutaifunga Argentina, bila shaka. Ndani na nje ya uwanja, ikiwa itabidi, nitafunga goli na kuchukua kila kitu”.

Lakini mambo yalibadilika kwa upande wao na kushuhudia Argentina wakichomoza na ushindi na yakifungwa na Julian Alvarez dakika ya 4, E. Fernandez dakika ya 12′, A. Mac Allister 37′ na G. Simeone dakika 71′ huku goli la pekee la Brazil likifungwa na M . Cunha dakika ya 26′.

Brazil imekuwa na rekodi mbaya hivi karibuni hasa wanapokutana na Argentina ambapo kwenye mechi 5 za mwisho zote wamepoteza kwa kuruhusu magoli 7 na wao kufunga goli 1 pekee.

Pia mchezo huo ulishuhudia kinda Giuliano Simeone akifunga goli lake la kwanza kwenye timu yake ya Taifa ya Argentina.

#NTTupdates