Na Mwandishi wetu.
Leo Januari 24, 2025 ni siku ya nne, tangu kuzinduliwa kwa Kliniki maalumu ya ushauri wa kisheria bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro huku idadi kubwa ya wananchi wakiendekea kujitokeza kwaajili ya kupata huduma hiyo ya ushauri wa kisheria.
Kliniki hiyo ilizinduliwa mnamo Januari 21, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nudrin Babu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Kamati ya ushauri wa kisheria ya Mkoa wa Kilimanjaro ambapo RC Babu aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe elimu ambayo itawasadia kupunguza migogoro mbalimbali inayowakabili.
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Joseph Shoo amesema kuwa muitikio wa wananchi wanaoendelea kufikia katika viwanja hivyo vya Stendi ya vumbi umekuwa ni mzuri huku akielezea masuala ambayo wananchi wengi wamekuwa wakihitaji ushauri wa kisheria ni masuala kama ndoa, ardhi, mirathi na masuala ya kijinsia ambayo wananchi wengi wameyalalamikia.
Kwa upande wao wananchi waliokwisha kupatiwa huduma hiyo ya msaada wa kisheria wameiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kufanya kitu hicho mara kwa mara ili kila mwananchi apate kujua haki yake huku wakisema kuwa wapo wananchi wengi vijijini wanapoteza haki zao kwa ukosefu wa kutokujua sheria na kuwaomba wainginie maeneo ya vijijini pia kutoa elimu hiyo.
#NTTupdates.