Na Mwandishi wetu.
Rais wa heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji “MO” ameweka Bonus ya Milioni 500 kwa wachezaji kama watafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) leo na kuwaondoa Al Masry.
Pia matajiri wengine na Viongozi wa klabu hiyo wametoa ahadi ya Milioni 3 kwa mchezaji ambaye atatoa pasi itakayozaa goli (Assist) kwenye mchezo huo ili kuondoa uchoyo na ubinafsi ambao iliwakosesha ushindi kwenye mchezo wa kwanza pale Misri baada ya kufungwa magoli 2-0 licha ya kupata nafasi nyingi za kuweka mpira kambani lakini walishindwa.
#NTTupdates