×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KWA BONUS HII MNYAMA ANABEBA

Na Mwandishi wetu.

Kuelekea mchezo mkubwa wa fainali ya mkondo wa kwanza kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), kati ya RS Berkane ya Morocco dhidi ya Mnyama Simba SC ya Tanzania mabosi wa klabu hiyo wametoa ahadi ya bonus ya kutosha kwa wachezaji hao kama watafanikiwa kushinda mchezo huo.

Tajiri Mohamed Dewji “MO” ameahidi benchi la ufundi na wachezaji wote wa klabu hiyo kama watafanikiwa kubeba taji hilo watapewa bonus ya kiasi Cha Bilioni moja kama zawadi ya ushindi huo.

Simba SC atashuka dimbani majira ya saa 4:00 usiku katika uwanja wa Berkane Municipal kucheza mchezo huo huku matarajio yao kupata matokeo mazuri ili waweze kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa fainali ya mwisho itakayopigwa Tanzania Mei 25, 2025.

#NTTupdates