Na Mwandishi wetu.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Inter Milan ya Italia, Lautaro Javier Martinez (27), ametoa lawama zake kwa wachezaji wenzie baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye mashindano yanayoendelea ya kombe la Dunia ngazi ya vilabu la FIFA nchini Marekani, baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya 16 bora hapo jana kwa kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Flumenense ya Brazil.
“Nataka kupigania mataji makubwa, Nani anataka kubaki Inter vizuri sana na tupambane, Nani hataki kubaki, wanaweza kwenda na kuondoka “.
“Tunahitaji wachezaji ambao wanataka kuwa hapa, Tumevaa jezi muhimu, Tunahitaji watu wenye uwezo wa hali ya juu au tafadhali, ondokeni”
Martinez amewalaumu baadhi ya wachezaji wenzie ndani ya Inter Milan kuwa hawajitumi wala kuipambania jezi ya timu hiyo akiwataka waondoke kwa vile hawana mchango ndani ya klabu hiyo.
#NTTupdates