Na Mwandishi wetu.
Baada ya kuwepo kwa taarifa ya klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kutaka kuvunja mkataba na nyota Neymar Jr (32) kutokana na Majeraha anayoyapata mara kwa mara na kuwepo kwa taarifa nyingine kuwa nyota huyo huenda atarejea nyumbani kwao Brazil na kujiunga na Palmeiras inayoshiriki ligi kuu Brazil.
Rais wa Palmeiras Leila Pereira amekanusha taarifa hiyo na kusema “Neymar hatajiunga na Palmeiras, klabu hii sio idara ya matibabu, Nataka mtu ambaye atakuja kujiunga mara moja na anaweza kucheza hata kesho ikiwa meneja anataka”.
“Sitakubali kusajili mchezaji ambaye hastahili kucheza ni mchezaji mkubwa labda atajiunga na Santos klabu yake ya utotoni”
Rais huyo amevunja ukimnya akiwataka mashabiki wa Palmeiras kuondoa matumaini na uvumi ulioenezwa kuwa nyota huyo atajiunga na klabu hiyo.
#NTTupdates