×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

LISSU AHOJIWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU

Na Mwandishi wetu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu amefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA – Taifa, amefikishwa Mahakamani hapo Leo majira ya saa kumi na robo Alasiri na kuwekwa Moja Kwa Moja kwenye Mahabusu ya Mahakama hiyo.

Lissu amekamatwa hapo haja huko Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma muda mchache baada ya kumaliza kuhutubia Mkutano wa hadhara na Kisha kusafirishwa hadi Jijini Dar es Salaam, kabla ya kifikishwa Katika Mahakama hiyo.

Lissu Tayari amehojiwa Katika Kituo Kikuu Cha Polisi Central Jijini humo.

#NTTUpdates