×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

LIVERPOOL YAIKANDA MADRID 2-0 UEFA

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Liverpool imepata ushindi mnono dhidi ya Mabingwa wa kihistoria wa Ulaya, Real Madrid kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Magoli ya Liverpool yamefungwa na kiungo mshambuliaji Alexis Mac Allister dakika ya 52 na mshambuliaji Cody Gapko dakika ya 77 na kupeleka ushindi huo na furaha kwa mashabiki wa Liverpool.

Mchezo huo ulishuhudia pia mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappe akipoteza mkwaju wa penati baada ya goli kipa wa Liverpool Caoimhin kelleher kuzuia mpira huo kuingia nyavuni kwake.

Real Madrid imeendelea kusuasua kwenye mashindano hayo na huenda wakashindwa kutinga hatua ya mtoano.

#NTTupdates