×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MADINI YAIPAISHA SHINYANGA, YAKUSANYA MABILIONI

Na Mwandishi wetu.

Makusanyo ya maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini katika Mkoa wa Shinyanga yatokanayo na mrabaha, tozo na ada mbalimbali kwa mwaka wa fedha ulioanza Julai 2024/ 2025 ni Shilingi Bilioni 21.5 Mkoa wa Shinyanga ulipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 26.2 ambapo mpaka mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu umefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha ambacho ni sawa na asilimia 123 katika kipindi cha miezi nane na asilimia 82 ya lengo la mwaka.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mjiolojia Daniel Mapunda amesema fedha hizo zimekusanywa kutokana na jitihada mbalimbali walizofanya katika usimamizi wa sekta.

“Mwenendo ni mzuri, hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha tuna imani tutafikia lengo,” amesema Mapunda.Aidha, Mapunda ametoa wito kwa wawekezaji kote nchini kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini mkoani Shinyanga ambao una utajiri mkubwa wa madini ya Almasi, Dhahabu na Madini Ujenzi.

“Mkoa wa Shinyanga tuna shughuli mbalimbali za madini ambazo zinajumuisha utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini;…. “Shughuli hizi zinafanyika kwenye wilaya zote mbili, Kishapu na Shinyanga.

“Tuna migodi mikubwa miwili wa kati mmoja na leseni 375 za uchimbaji mdogo na katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/ 2025 tumetoa leseni ndogo za biashara ya madini 51 na leseni kubwa za biashara ya madini 21 amesema Mapunda.

Amesema, pia zipo fursa za uchenjuaji wa madini na kwamba wana jumla ya mitambo 150 ya uchenjuaji katika maeneo yanayosimamiwa na Tume ya Madini katika Wilaya za Kishapu na Shinyanga.

#NTTUpdates