Na Mwandishi wetu.
Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza maduka yanayokadiriwa kuwa kumi na Saba (17 )katika eneo la Buseresere wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo ulianzia usiku wa kuamkia leo June 11, Katika moja ya duka lenye vifaa vya umeme na hatimae kusambaa katika maduka mengine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Hamis Dawa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema taarifa zaidi ya kutokea Kwa moto huo itatolewa .
#NTTUpdates