Na Mwandishi wetu.
Taarifa rasmi ya kutoka vyombo vya usalama nchini Myanmar ( Burma) vimeripoti Watu zaidi ya 1,600 wamepoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7.7 lilitokea katika maeneo mengi ya nchi hiyo siku ya Ijumaa Machi 28, 2025 na kuathiri mataifa jirani na nchi hiyo.
Pia Maelfu ya watu wamejeruhiwa nchini Myanmar kutokana na kadhia hiyo ambapo vyombo vya usalama na uokoaji vinaendelea kutoa misaada na kuwatafuta watu wengine ambao wamekwama kwenye vifusi vya maghorofa yaliyoporomoka.
Uongozi wa kijeshi nchini Myanmar imeomba misaada ya vifaa vya kisasa na wataalam wa uokoaji kutoka mataifa mengine kuwasaidia ili kuwaokoa watu ambao wameathiriwa na kadhia hiyo.
#NTTupdates