Na Mwandishi wetu.
Mafundi ujenzi Mkoani Mwanza, wameiomba serikali kuondoa Changamoto ya ukosefu wa mitaji, vifaa vya kisasa na upungufu wa Fursa za dhabuni ambazo zimekuwa zikwamisha mafundi wengi kusonga mbele Katika shughuli zao.
Wameyasema hayo Wakati wa ufungaji wa elimu ulio washirikisha mafundi zaidi ya 2500 ambapo waliomba serikali Kupitia wizara ya viwanda na wizara ya ujenzi kuangalia uwezekano wa kuwezesha vikundi vya mafundi wa ndani kupata Fursa za ujenzi wao kama mafundi wa ndani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Magic Bulders David Balongo amesema kuwa wanao zaidi ya mafundi laki saba nchini na wanatamani kuona mafundi hao wanakuwa matajiri kupitia shughuli zao wanazofanya
Naye mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema Serikali imeandaa kiasi Cha shilingi trioni 5.6 kwaajili ya sekta ya ujenzi na mawasiliano na wao kama serikali ya mkoa itaendelea kutoa Fursa za ujenzi kwa mafundi wazawa ambao wamekuwa wakichochea ukuwaji wa pato la Taifa na maendeleo ya miradi ya miundombinu.
Mtanda ameongeza kuwa serikali inao utaratibu wa manunuzi wa mafundi, kuomba tenda na wao kama mkoa wanatarajia kuandaa mafunzo ya kuwaelimisha namna ya uombaji wa dhabuni za serikali ambao imekuwa Changamoto kwa Baadhi ya mafundi ujenzi
#NTTUpdates