Na Mwandishi wetu.
Kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 nchini Tanzania, Wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wametakiwa kuwa makini kwa kufanya kazi hiyo ya usimamizi kwa weledi kwa kuzingatia Sheria pamoja na taratibu za uchaguzi.
Hayo yamesemwa na hii leo Novemba 22, 2024 na Bi. Rose Mhina ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi kwa niaba ya Bi. Happiness R. Laizer ambaye ni msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Monduli katika ukumbi wa shule ya msingi Losirwa.
Bi. Rose Mhina amewataka wasimamizi hao kuzingatia viapo vyao kwani kazi hii inahitaji uaminifu na uadilifu mkubwa ili uchaguzi huo uwe wa huru na haki kama ambavyo taratibu zinavyoelekeza.
Kwa upande wake, Bi. Sarah Andrew Lombo ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo yaliyotolewa hii leo amesema kuwa wapo tayari kwaajili ya zoezi hilo muhimu kwa siku hiyo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
#NTTupdate.