Na Mwandishi wetu.
Rais mteule wa Chama Cha Madaktari wa mfumo wa mkojo Tanzania(TAUS), Doctor Deogratias Emmanuel Mahenda amesema kuwa, magonjwa ya mfumo wa mkojo Kwa asilimia kubwa yamekuwa yakiwasumbua wanaume ikiwemo tezi dume, UTI, saratazi ya tezi dume na saratani ya kibofu Cha mkojo ambapo kwa asilimia kubwa magonjwa ya tezi dume uwapatana watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Amesema Kwa Mwaka 2024 walifanya zoezi Hilo Kwa kushirikiana na hospitali ya Mloganzila ambapo walilenga uondoaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kupitia matundu madogo huku Kwa mkoa wa Dodoma walilenga kuondoa matatizo ya nguvu za kiume ambapo waliweka vipandikizi Kwa wale ambao hawana nguvu za kiume ili waweze kufanikiwa kufanya tendo.
Ameyasema hayo Jijini Mwanza katika kambi ya Madaktari bingwa wa njia ya mkojo iliyowekwa katika viwanja vya Furahisha kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi jijini humo.
Aidha Dkt Mahenda alitoa wito kuwa ni Muhimu wananchi kuwahi Katika vituo vya afya pale wanapokundua kuwa wanamagonjwa ya mfumo wa mkojo ili waweze kupata matibabu mapema kwani magonjwa hayo utibika na wanapoona wito wa matibabu ya Bure wawe na mazoea ya kuchangamkia fursa hizo maana afya ndio mtaji wa kwanza wa Mwanadamu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika katika kambi hiyo kwaajili ya uchunguzi wameiomba Serikali kupunguza gharama za matibabu Katika vituo vya afya pamoja na Kuongeza upatikanaji wa huduma rafiki Kwa baadhi ya huduma ambapo zimekuwa zikisumbua wananchi wenye kipato Cha chini kushindwa kumudu kupata huduma za matibabu hususani za kibingwa.
#NTTUpdates