ร—
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAJALIWA ALAANI TABIA YA UKWEPAJI WA KODI

Na Mwandishi wetu.

Wazari Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amelaani vikali tabia ya ukwepaji wa kulipa kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni nchini akisema kuwa hali hiyo inaikwamisha Serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Majaliwa amesema hayo leo Julai 08, 2025 wakati akifungua mkutano wa mwaka wa tathimini ya utendaji kazi wa TRA, unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano Arusha ( AICC)

Majaliwa amesema wafanyabiashara hao wa kigeni wameanzisha bohari ambazo zinaingiza mizigo bila udhibiti, na wanaendelea kufanya biashara kubwa bila kuzingatia sheria za kodi.

Ameongeza kuwa mataifa mengine yana sheria kali za kodi kwa wageni, na Watanzania wanaokwenda kufanya biashara nje wanalazimika kuzingatia sheria hizo, hivyo wageni wanaofanya biashara nchini ni vyema wakatambua na kuheshimu sheria za kodi za ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuimarisha ukaguzi na uchunguzi dhidi ya wageni wanaofanya biashara nchini. “TRA mna wachunguzi, nendeni mkachunguze hawa wanaokuja kufanya biashara nchini.

Wanakuja na kuondoka na mapato yetu. Lazima tubane eneo hilo kama na sisi tunavyobanwa tunapokwenda kwao. Wala hakuna haja ya kubainisha nchi yeyote, aliyeamua kuja kufanya biashara nchini lazima ajue kuna sheria,” amesema Waziri Mkuu.

#NTTupdates.