×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA DKT. NDUGULILE

Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 03, 2024 ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya DunianiKanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile yaliyofanyika eneo la Mwongozo, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine walioshiriki Mazishi hayo ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Wazir wa INchi, Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na viongozi wa Chama na Serikali.

Dkt. Ndugulile alifariki usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

#NTTUpdates