Na Mwandishi wetu.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua nembo na kauli mbiu ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania huku akisisitiza watanzania wote kueendelea kuulinda na kuuheshimu Muungano ambao umeendelea kukuza udugu .
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa Nembo na Kauli ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Muungano ambapo kauli Mbiu ya maadhimisho hayo inasema”tumeshikamana, tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu”.
“hafla ya leo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano,Katika siku ya leo tunashuhudia nchi yetu inaanza safari ya kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sherehe hizi za uzinduzi wa nembo na kaulimbiu zitakazotumika katika maadhimisho ya mwaka huu,
Hivyo basi leo tumekutana kwa lengo mahsusi la kushuhudia uzinduzi wa nembo na kaulimbiu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano,Hatuna budi sote kuwashukuru sana viongozi wetu kwa kuwezesha muungano wetu kufikia umri huu wakati Watanzania wote tukiwa bado tuna umoja na mshikamano wa Kitaifa,”amesema Waziri Mkuu.
NttUpdates