Na Mwandishi wetu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini mara mbili katika nafasi muhimu za uongozi wa umma.
Akizungumza leo Juni 24, 2025, wakati wa Jukwaa la Wanawake Arusha lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Makonda amesema hakutarajia hotuba hiyo ingekuwa ya kuaga.
“Balozi (Dkt. Emmanuel Nchimbi) naomba kwa unyenyekevu mkubwa unifikishie salamu kwa Rais Samia kwa kuniamini mara mbili ndani ya utumishi wake wa urais tangu mwaka 2021 kuniteua kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Sikutarajia leo itakuwa hotuba yangu ya kuaga,” amesema MakondaMgeni rasmi katika jukwaa hilo la Wanawake Arusha alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Katika mabadiliko madogo ya viongozi yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu hapo jana, Kenan Kihongosi amehamishwa kutoka kuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha, akichukua nafasi ya Makonda.
#NTTupdates.