ร—
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MALALAMIKO YA KODI YAMEPUNGUA KWA WAFANYABIASHARA โ€“ DKT. NCHEMBA

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameeleza kuwa malalamiko ambayo yalikuwa yakitolewa na wafanyabiashara kuhusu taratibu za ukusanyaji wa kodi, yamepungua kwa kiwango kikubwa, jambo linaloashiria kuwa mfumo wa ukusanyaji sasa unaeleweka na kukubalika zaidi kwa wafanyabiashara wote nchini.

“Nikiri kwamba makusanyo yameongezeka… kulikuwa na nyakati ambapo nilikuwa napokea malalamiko mengi kutoka kwa wabunge na wafanyabiashara walipa kodi.

Nikiri makusanyo yameongezeka kwa kiwango kikubwa sana, na malalamiko pamoja na manung’uniko yamepungua sana, karibu yameisha. Kwa hivyo, tunaelekea katika hatua ya kufanya ukusanyaji wa kodi kuwa jambo la maendeleo ya nchi badala ya uadui,” amesema Dkt. Mwigulu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Nchemba ameitaka Mamlaka hiyo kuendelea kufikiria namna bora ya kuwadhibiti wale wote ambao wanakwepa ulipaji wakodi akisema kuwa kwani bado wapo wafanyabiashara ambao hawalipi kodi na wala biashara zao hazijasajiliwa, wapo wanaouza bila ya kutoa risiti hao wote wanapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu ili wawekwe kwenye mfumo wa ulipaji kodi kama wafanyabiashara wengine.

Dkt. Nchemba amesema hayo leo, Julai 8, 2025, katika mkutano wa mwaka wa tathmini ya utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unaofanyika jijini Arusha, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya mamlaka za kodi na walipa kodi unaleta faida kwa Taifa.

#NTTupdates.